Jeshi la polisi Tanzania limetolea ufafanuzi taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii kutoka ubalozi wa Marekani ikionyesha kuwa na uwezekano wa kigaidi nchini na kwamba limeanza kufanyia kazi taarifa hiyo.
Katika taarifa iliyotolewa leo Januari 26, 2022 na Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu Dodoma, David Misime inasema taarifa hiyo ilisambaa jana.
Aidha taarifa hiyo inasema pale itakapo bainika jambo lenye kutia shaka au kuonekana mtu/watu wenye kutia mashaka kutokana na mienendo taarifa hizo ziripotiwe.
Chanzo: Mwananchi