Polisi Watanda Kanisa la Kijitonyama Aliposimamishwa Mchungaji


SAKATA la kusimamishwa kazi kwa Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Usharika wa Kijitonyama, Dk. Eliona Kimaro, limeendelea kuwa gumzo huku askari wakionekana kufanya doria kanisani huko.

Juzi usiku kwenye ibada ya 'masifu ya jioni', askari polisi walionekana wakizunguka nje ya kanisa hilo wakati ibada ikiendelea ndani ya kanisa.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, alipozungumza na Nipashe kuhusu suala hilo, alisema doria za askari polisi ni za kawaida kwenye maeneo mbalimbali ya jiji hilo la kibiashara.

"Nikuulize kabla ya hilo sakata, hukuwahi kuona askari wakizunguka kanisani hapo? Hizi ni doria za kawaida na haihusiani na jambo hilo," alisema Kamanda Muliro.

Ikiwa ni siku ya nne tangu kuibuka kwa mvutano huo, juzi Nipashe iliwashuhudia waumini wakiendelea kufanya ibada nje ya kanisa wakati ibada ya masifu ya jioni hufanyika ndani ya kanisa.

Wakiwa nje ya kanisa hilo, waumini hao waliimba nyimbo za kumsifu Mungu na kumwombea Mch. Kimaro.

Katika kuhakikisha usalama unaimarishwa kwenye kanisani hilo, kila aliyekuwa anaingia, getini aliulizwa majina na namba za mtaa anaotoka.

Mchungaji Kimaro alisimamishwa kuendelea na huduma ya kichungaji katika usharika huo kwa siku 60 pasi na kuwekwa wazi sababu za adhabu hiyo.

Tangu Jumanne uongozi wa Dayosisi hiyo umekuwa ukitafutwa na waandishi wa habari kuzungumzia sakata hilo bila ya mafanikio.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad