Rais Samia Amemteua David Kafulila na Wengine



Rais Samia amemteua David Kafulila kuwa Kamishna wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP). Kafulila ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu mstaafu.

Rais Samia pia amemteua Justine Mwandu, kuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC). Mwandu ni Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Tanzania Reinsurance (TANRE).

Aidha Rais Samia amemteua Profesa Verdiana Grace Masanja, kuwa Mwenyekiti wa taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI). Masanja ni Profesa wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela

Mwingine aliyeteuliwa ni Griffin Venance Mwakapeje, kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya kurekebisha sheria Tanzania, ambapo awali alikuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma, Wizara ya Katiba.

Mwakapeje anachukua nafasi ya Casmir Kyuki ambaye atamaliza kipindi chake Januari 7, 2023.

Na mwisho amemteua Fatma Mohamed Abdallah, kuwa Mkurugenzi wa Puma Energy Tanzania. Fatma Mohamed Abdallah ni Meneja wa kampuni ya Puma Energy nchini Geneva na anachukua nafasi ya Dominic Dhanah ambaye amemaliza muda wake.

B

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad