Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali nchini wakiwemo wenyeviti wa bodi na Makamishna kadhaa
Rais Samia amemteua Prof. Ahmed Mohamed Ame kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) akichukua nafasi ya Mhandisi John Ndunguru
Amemteua Eliud Betri Sanga Kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Airtel Tanzania
Aidha Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Jaji (Mstaafu) Mathew Mhina Kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Mohamed Khamis Hamad kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kipindi cha pili
Kwa upande wa Makamishna Rais Samia amewateua Nyanda Josiah Shuli, Khatibu Mwinyi Khatibu, Amina Talib Ali ma Thomas Paulo Masanja kuwa Makamishna wa wa Haki za Binadamu na Utawala Bora