Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema baada ya kutoa rukhsa ya mikutano ya hadhara huenda wapo ambao watakuja na kasi ya malumbano hivyo amewaomba Vijana wa CCM wasiende kulumbana bali wajibu hoja kwa takwimu, ushahidi n.k.
Akiongea na Vijana kwenye Kilele cha Matembezi Maalum ya UVCCM ya kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi Zanzibar, Rais Samia amesema “Ukisema kwa ustaarabu na kuchagua ya kusema wewe unajiamini na kama unajiamini huna haja ya kupayuka, unajibu hoja kwa kujiamini na ushahidi lakini unapobwawaja na kupayuka ni ishara ya uoga, niwaombe Vijana wa CCM msiende kupayuka nendeni kajibuni hoja”
"Tunapokosolewa tuangalie yale ya kweli tuyachukue tuyafanyie kazi ambayo sio ya kweli tujibu hoja, sasa niwaambie zama za ugomvi, kupigana na kutukanana katika siasa sasa ziishe, twendeni na hoja za maana na za kujenga, tuvumiliane tulete maendeleo ya kweli na yenye tija ili tujenga Tanzania mpya yenye maendelea endelevu, Taifa lenu linawahitaji"