Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya akiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo Jumatatu Januari 9,2023. Picha na Janeth Mushi
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Herieth Mhenga amesema kwa kuwa matangazo ya hati ya wito yameshatolewa rufaa hiyo itaendelea kusikilizwa Januari 17.
Arusha. Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imepanga Januari 17, 2023 kuendelea na usikilizwaji wa rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kupinga hukumu iliyomwachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake.
Rufaa hiyo namba 155/2022, inapinga hukumu kesi ya uhujumu uchumi iliyowaachia huru Ole Sabaya na wenzake ambao ni pamoja na Enock Mnkeni, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.
Akiahirisha rufaa hiyo kwa niaba ya Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, leo Jumatatu Januari 9, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Herieth Mhenga, amesema kwa kuwa matangazo ya hati ya wito yameshatolewa rufaa hiyo itaendelea kusikilizwa Januari 17.