Ukweli ni kwamba watu wenye vipaji ni wengi mtaani, lakini hawajui waanzie wapi kwakuwa ‘gemu’ ya muziki tayari ina magwiji, ndivyo ilivyokuwa kwa mrembo #Anjella miaka michache nyuma kabla ya kupokelewa na #Harmonize mwaka 2021, wakati huo akifanya cover za nyimbo mbalimbali bila kufahamu hatima ya kipaji chake nani atakaye mshika mkono.
Ndipo kijana wa #Chitoholi aligungua kipaji cha #Mrembo na kuona kuna kila sababu ya kumsogeza mjini pongezi zikawa nyingi sana kutoka sehemu mbalimbali kwenda kwa #KondeBoy lakini leo hii mambo yamegeuka si pongezi tena zimekuwa lawama baada ya Anjella kuondoka #KondeGang.
Waungwana hakuna sababu ya kumlaumu #Harmonize kuwa hakutimaza vingi kwa #Anjella, ikumbukwe kuwa nyuma hakuna aliyekuwa akimfahamu Anjella lakini kupitia #Harmonize leo hii mtaani ngoma nyingi zinalia zenye sauti tamu ya #Anjella.
Anjella wa leo sio yule wa 2020 aliyekuwa anafahamika mataani kwao tu, huyu wa sasa tayari watanzania wanamfahamu na kumuamini kupitia kipaji chake, wakati wa kutofautisha hayo ndio wakati wa kumpongeza #KondeBoy kwa jitihada zake za kumtambulisha kwa watanzania na nchi jirani.
Inatakiwa ifike mahali jamii ielewe kuwa maisha ni safari na hatua moja huanzisha nyingine bila kutoa lawama kwa mtu yeyote yule, bila kuwaza zile ahadi za #Kode kwa #Anjella kutotimia, bila kusahau purukushani za kunyang’anyana account za mitandao, isisahaulike kuwa umuhimu wa #Konde kwa Anjella bado ni mkubwa sana.
Anjella ni kati ya wasanii wa kike ambao wakisimama kwenye vipaji vyao wanauwezo wa kufika mbali.
Hadi sasa Anjella tayari sauti yake inasikika kwenye nyimbo zaidi ya nane zikiwemo zake mwenyewe huku nyingine akiwa ameshirikishwa na wasanii mbalimbali, pongezi kwa #Harmonize kumtambulisha #Anjella kwa watanzania pia hongera #Anjella kwa kuonesha kipaji chako kwa watanzania.
.
Imeandikwa na @officialtinana