Said Nassor, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS)
RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Hussein Katanga kuwa Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa Mjini New York akichukua nafasi ya Profesa Gaston ambaye amerudishwa nchini.
Amesema mabadiliko ya uongozi katika ubalozi huo ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuhakikisha balozi za Tanzania zinafanyiwa maboresho ili kurudisha hadhi za balozi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Pia amemteua Said Nassor kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS).
Nassor amechukua nafasi ya Diwani Athuman ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Ikulu.
Rais Samia amefanya mabadiliko hayo tarehe 3 Januari, 2023 na kuyatangaza moja kwa moja kupitia televisheni.
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu Usalama wa Taifa, Diwani Athuman Msuya
Aidha, nafasi ya Balozi Katanga ambaye alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi, imechukuliwa na Moses Kusiluka ambaye awali alikuwa Katibu Mkuu Ikulu.
“Mtakumbuka Novemba mwaka jana kulikuwa na mjadala mkubwa bungeni kuhusu matumizi ya fedha na madaraka katika balozi zetu na kwa kuanza nimefanya mabadiliko katika ubalozi wetu wa kudumu mjini New York,” amesema.
Amesema amemteua balozi Katanga kutokana na uzoefu wake katika masuala ya kimataifa, uzalendo na hekima na busara katika uongozi.