Serikali ipunguze Ushuru Bidhaa za Hoteli


Wadau wa uwekezaji kwenye biashara ya hotelia wameomba Serikali endapo itawezekana kupunguza baadhi ya ushuru katika baadhi ya vifaa na bidhaa wanazoagiza kwa matumizi ya hoteli ikiwemo vifungashio vya chakula na vinywaji kwa kipindi hiki tu ambacho hoteli nyingi zimeathiriwa.


Mapema hii leo tumezungumza na mdau na mfanyabiashara katika sekta ya hoteli na vinywaji ambaye amesema kwa kipindi chote cha uviko 19 sekta iliyumba na wawekezaji kulazimika kupunguza baadhi ya watumishi huku kwa kipindi chote biashara ikifanyika kwa wazaw3a kutokana na watalii wengi kusalia katika nchi zao.


Robert Antony mdau wa sekta hiyo amesema wawekezaji wengi wa hoteli zilizoko katika fukwe wamekuwa wakipatiwa ushirikiano mkubwa kutoka kwa taasisi zingine za mazingira,chakula na dawa pamoja na vyombo vya ulinzi katika kuhakikisha wageni wanaofika wanakuwa salama wasio na madhara.


Pia amewataka wawekezaji wengine wazawa kwenye upande wa hotelia kuacha ujanja wa kuficha taarifa za mapato kwa mamlaka za kukusanya kodi kwa kuwa unapodai huduma wajibu wako kama mfanyabiashara ni kuweka kumbukumbu zako sawa.


Ameweka wazi kuwa uzinduzi wa filamu ya Royal tour uliofanywa na Rais DK Samia Suluhu Hassanulirejesha matumaini na kufufua sekta ya utalii kwa kasi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad