Simba Yavuliwa Ubingwa wa Mapinduzi Cup kwa Kipigo cha Mlandege




Kikosi cha Simba jana kimeanza Michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kupoteza baada ya kufungwa bao moja dhidi ya Mlandege katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Amaani huko Unguja VisiwaniZanzibar.

Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu huku lakini Simba walifika zaidi langoni kwao ila walikosa umakini wa kutumia nafasi walizotengeneza.

Mlandege wao walifanya mashambulizi machache ya kushtukiza lakini hata wao walikosa umakini kwenye eneo la mwisho la kumalizia. Bao pekee la mchezo huo limefungwa na kiungo Aboubakar Mwadini kwa kichwa dakika ya 75 akimalizia mpira wa kona.


Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa Nelson Okwa, Michael Joseph na Kibu Denis na kuwaingiza Victor Akpan, Joseph Mbaga na Hassan Mussa lakini mabadiliko hayo hayakuzaa matunda mpaka dakika ya 90 Maningwa watetezi wa Kombe hilo, Simba wakitoka vichwa chini baada ya kipigo.

Simba wamevuliwa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi baada ya kupokea kipigo hicho kutoka kwa Mlandege ambao wamefikisha alama 4 katika kundi lao, huku KVZ FC wakiwa na pointi 1 na Simba wakiwa hawana pointi na wakiwa wamesaliwa na mechi moja mkononi ambayo hata wakishinda watapata pointi 3 nyuma ya Mlandege.

Mchezaji wa Mlandege, Abubakar Mwadin ameibuka kuwa Mchezaji bora wa mchezo huo. Mwadin amekabidhiwa kitita cha Tsh. 500,000/- (Laki Tano) kutoka NIC.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad