Singida BS yaichapa Azam, mabao yaamua nafasi



MATOKEO ya ushindi wa bao 1-0 iliyopata Singida Big Stars dhidi ya Azam FC, haujabadili chochote kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.
Licha ya SBS inafanana pointi 43 na Azam FC na michezo ya kushinda 13, sare nne,  lakini itasalia nafasi ya nne kwa utofauti wa mabao 12.
SBS imecheza mechi 21, imeshinda 13, sare nne na imefungwa michezo minne,inamiliki mabao 24, imetikiswa nyavuni mara 15 na ina pointi 43.
Azam FC imecheza mechi 21, imeshinda 13, sare nne, imefungwa mechi minne, ina mabao ya kufunga 36 mabao ya kufungwa 21 na ina pointi 43.

Singida Big Stars ilipata bao  dakika ya 45+ ambapo Bruno Gomes alipiga faulo nje ya boksi shuti lake likamshinda kipa wa Azam FC, Ali Ahamada.

Mzunguko wa kwanza Singida Big Stars, ilipoteza Uwanja wa Chamazi kwa bao 1-0 ambalo lilifungwa na Sospeter Bajana dakika 47 akipokea pasi ya mwisho ya James Akaminko, hivyo hizo timu kila moja imeshinda kwenye uwanja wake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad