Tanasha "Siwezi Kuwa na Mwanaume Anayenuka Jasho, Oga Mara Tatu Kwa Siku"



Mwimbaji wa muziki na mwanamitindo kutoka nchini Kenya, Tanasha Donna amesistiza kuwa usafi kwa wanaume na wanawake ni lazima.


Tanasha ambaye ni mzazi mwenza na msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesema kuwa kwa mtu yeyote haijalishi anapitia changamoto gani katika maisha, lakini ahakikisha unanukia vizuri popote uendapo.


Kupitia video fupi aliyoipakia Instagram, mwanamuziki huyo alifafanua kwa mapana jinsi watu wanafaa kudumisha usafi katika miili yao na mazingira wanamoishi.


Alisema kuwa kwa mtu yeyote haijalishi unapitia changamoto gani katika maisha, lakini hakikisha unanukia vizuri popote uendapo, na si tu kwa kujipulizia marashi bali kwa kukoga mwili mara mbili hadi mara tatu kwa siku bila kusahau kupiga mswaki na kuvalia nadhifu muda wote.


“Sijui ni mara ngapi tutalizungumzia hili lakini watu wangu, wanawake kwa wanaume, usafi ni kitu cha muhimu sana. Ni muhimu sana watu wangu kama hamkuwa mnajua,” Tanasha Donna alianza kushauri.


“Hakikisha unanukia vizuri si tu kwa kujirembesha kwa marashi kwa nje, lakini usafi halali. Hakikisha unanawa mikono yako, usisahau kufanya utaratibu wa kukoga kati ya mara mbili na mara tatu kwa siku, piga mswaki, tumia kopo la msalani vizuri na pia osha kwa maji baada ya kumaliza kukata gogo. Nyoa nywele zote mwilini mwako, kaa nadhifu,” alisema Tanasha.


Ameendelea kwa kusema “Natumai wengi wenu mmesikia nukuu kuwa usafi humweka mtu karibu na kumcha Mungu, ni ukweli watu wangu. Utagundua kuwa kukiwa na uchafu karibu nawe unapoteza dira ya akili lakini wakati kuna usafi unahisi mwenye utulivu na amani. Miili yetu ni hekalu takatifu la Mungu, tuilinde wote wake kwa wanaume,” Alisema.


Vile vile, mwanamuziki huyo alisema yeye hawezi kubaliana na wale wanaosema ‘mwanaume ni jasho’ huku akisema kudumisha usafi ni kwa watu wote.


Alizidi mbele kunukuu kifungu maarufu kutoka kwa Biblia kinachosema kuwa usafi unamweka mtu karibu ya ucha Mungu akisema kuwa kama hakuna usafi karibu nawe, huwa unakosa hata utulivu wa akili.


“Natumai wengi wenu mmesikia nukuu kuwa usafi humweka mtu karibu na kumcha Mungu, ni ukweli watu wangu. Utagundua kuwa kukiwa na uchafu karibu nawe unapoteza dira ya akili lakini wakati kuna usafi unahisi mwenye utulivu na Amani. Miili yetu ni hekalu takatifu la Mungu, tuilinde wote wake kwa wanaume,” alisema Tanasha.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad