UKWELI Mchungu: Harmonize Amejitengenezea Mashabiki zake, Rayvanny Anatembelea Upepo wa Mashabiki wa Diamond


Kitaalamu zaidi Msanii mkubwa anapimwa kwa LEGACY, CONSISTENCY NA INFLUENCE.

Msanii hapimwi kwa Tuzo, Views, Likes, Followers wala Subscribes maana hizi data unaweza ukazinunua (watu kibao wananunua VIEWS, Followers, SUBSCRIBERS, N.K. Watu wananunua Tuzo. Muulize kila msanii anajua kwamba kuna ununuaji wa Tuzo)

Hivyo Msanii bora anapimwa kwa LEGACY, CONSISTENCY na INFLUENCE maana hivi huwezi Viiba wala kuvinunua.

Harmonize ameacha Alama/Legacy, leo hii ukimuona Anjella na Ibraah tayari unavuta picha ya Harmonize.

HARMONIZE amekuza Ideology ya "ukipambana utafanikiwa", Vijana wengi wanapambana kwa sababu wameona mtu kama Harmonize amepambana na Amefanikiwa, kutoka Kuuza Maji mpaka Ustar sio jambo, dogo. Kupitia nyimbo zake za Inspiration ameeleza mengi aliyopitia na kiukweli ame-inspire vijana wengine. Rayvanny hajawahi ku-ispire watu na hana nguvu hiyo.

Harmonize amekuwa na Muendelezo Mzuri kimuziki, Hashuki kabisa( ana CONSISTENCY) Ila Rayvanny tangu atoke WCB kuna vitu havipo sawa.

Harmonize ana ushawishi mkubwa, Harmonize amefanya Show kenya amejaza, Rayvanny hana uwezo huo. Harmonize anaweza akazunguka Kila mkoa na watu wakajaa uwanjani ila Rayvanny hana huo uwezo maana hana ushawishi.

Harmonize amefanikiwa kupata mashabiki zake, ila Rayvanny bado anatembelea upepo wa mashabiki wa Diamond, hana Mashabiki zake.

Tyga

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad