Tunathibitisha kutokea kwa kifo cha aliyekuwa mchezaji na kapteni wa timu yetu ya vijana (U17), Mohammed Banda, kilichotokea leo asubuhi Januari 19, 2023.
Banda alipoteza maisha alipofikishwa Hospitali ya Mkoa wa Singida baada ya kugongana kichwani na mchezaji mwenzake wakiwa mazoezini katika Uwanja wa Magereza, Singida.
Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu mzito.