Wafa Maji Wakupeana Raha Baada ya Gari Kutumbukia Majini



Tukio hili limetokea Kenya Jumatatu usiku. Mwanaume na mwanamke wamefariki dunia baada ya gari walimokuwa ndani kutumbukia kwenye bwawa liitwalo Titanic huko Juja, kaunti ya Kiambu nchini Kenya.

Miili yao inadaiwa kukutwa ikiwa utupu.

Taarifa zinadai kuwa walikuwa ‘wakifanya yao’ wakati wameegesha gari hilo pembezoni mwa bwawa. Wakiwa hawajui, gari likaanza kuseleleka pole pole hadi likatumbukia bwawani.

Mwanamke alifanikiwa kutoka nje ya gari, lakini kwakuwa hakuwa na divers alikufa maji.

Mke wa mwanaume huyo, amesema mumewe alikuwa mfanyabiashara na jioni ya Jumatatu alimweleza kuwa alikuwa na mkutano wa kibiashara huko Juja.

Kwa mujibu wa mashuhuda, wawili hao waliegesha gari mita chache kutoka kwenye bwawa hilo mida ya saa 3:30 usiku na walisikia watu wakipiga kelele kuomba msaada.

Mwili wa mwanaume uliondolewa bwawani Jumatano hii na kupelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti pamoja na mwili wa mwanamke huyo ambapo mke wake alimtambua.

“Ingawa simjui, naamini mwanamke huyo aliyekuwa na mume wangu alikuwa ni rafiki tu, [Mume wangu] alikuwa na marafiki wengi sababu ya asili ya kazi yake,” mke wa marehemu ameiambia Citizen TV.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad