Taarifa kutoka nchini Kenya zinaeleza kuwa Mwanamke mmoja alinaswa akifanya uchumba na mpenzi wake kwenye gari lake katikati ya Barabara ya Thika, na hivyo kusababisha mrundikano wa magari aswekwa Jela miezi sita jela na faini ya Ksh 20,000.
-
Akiwa amefikishwa mbele ya Mahakama ya Makadara mnamo Januari 24, mwanamke huyo alikiri kosa la kusababisha fujo na kuzuia trafiki katika Thika Road Mall huko Roysambu.
-
Hakimu alifahamishwa kuwa maafisa wa trafiki wanaosimamia barabara hiyo walishangazwa na msururu wa foleni.
Wakati wakitaka kujua chanzo cha msongamano huo, walimkuta mwanamke huyo akiwa katika mazingira ya kutatanisha na mwanamume aliyekuwa kwenye gari lao ambalo lilisimamishwa katikati ya barabara.
-
Polisi hao waliiambia mahakama kwamba walikatiza kitendo hicho kwa upole na kuwataka wapenzi hao watafute maeneo sahihi lakini wapenzi hao waliendelea.
-
Huku wakiwa wamekasirishwa na ombi la Maafisa hao, washtakiwa hao wanadaiwa walianza kuwarushia matusi maafisa hao waliokuwa na silaha na hata inasemekana walithubutu kufyatua risasi.
Maafisa waliripoti kisa hicho kilichotokea Januari 24 katika Kituo cha Polisi kutokea eneo la tukio.