Yanga imezindua Jezi Maalum Ambazo itazitumia Kwenye Mashindano ya Kombe la Shirikisho la CAF


Yanga imezindua jezi maalum ambazo itazitumia kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho la CAF [CAF Confederation Cup] 2022|23 kuanzia hatua ya Makundi.

Ukiangalia jezi hizo mpya, kifuani amewekwa mdhamini ambaye wamemtangaza leo, kampuni ya Haier zina kwa sababu mdhamini mkuu wa Yanga [kampuni ya michezo ya kubahatisha] hawataweza kumtumia kwenye mashindano ya CAF kuanzia hatua ya makundi.

Taratibu za masoko za CAF haziruhusu timu yoyote kuvaa jezi yenye mdhamini wa kampuni ya kubahatisha kwakuwa tayari CAF inadhaminiwa na kampuni ya michezo ya kubahatisha [wanazuia mgongano wa kimaslahi].

Ndio maana misimu kadhaa nyuma, Simba ilicheza huku jezi zao zikiwa hazina mdhamini kifuani lakini baadae wakaja na #VisitTanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Utalii ili kutangaza utalii wa Tanzania
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad