Adaiwa kumuua mfanyakazi wake wa ndani kisha kupeleka Hospitali



DIANA Joseph, mkazi wa Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam, anadaiwa kumuua msichana wake wa kazi za ndani Anne Kassim (20) na kisha kumpeleka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kudai kuwa amemkuta binti huyo amejinyonga bafuni.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Debora Magiligimba, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, amesema kuwa tukio hilo limetokea Februari 8, 2023 majira ya saa 2 usiku nyumbani kwa mtuhumiwa huyo.

Amesema Februari 9, mwaka huu majira ya saa 9:45 asubuhi Jeshi la Polisi lalipokea simu kutoka kitengo cha dharura Muhimbili kuhusu mwili huo kufikishwa hospitalini.

“Tulipokea taarifa kutoka kwa mkuu wa kitengo cha dharura kwamba saa 5 akiwa Muhimbili alipokea mwili wa Anne Kasssim akiwa amefariki dunia na uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi ambao ulitufikia ni kwamba alifikwa na umauti baada ya kujinyonga”

“Jeshi lilibaini hapakuwa na dalili zozote za marehemu kujinyonga na mpaka sasa Jeshi la Polisi Ilala, tunaendelea na uchunguzi kuhusu chanzo cha kifo na tunasubiri taarifa za daktari kufahamu kwa kina” amesema Kamanda Magiligimba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad