Afariki Dunia Akiombewa Kanisani




Kampala. Polisi nchini Uganda wanachunguza tukio la mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 59, Rosette Najuma ambaye ameaga dunia siku ya Jumatano Februari 8 wakati akifanyiwa maombiKanisa la Christian Life lililopo Makerere.

Kwa mujibu wa Msemaji Msaidizi wa Polisi wa Kampala, Luke Owoyesigyire amesema Najuma alizirai na kufariki wakati ibada ikiendelea katika kanisa hilo lililopo jijini Kampala.

Rosette anaripotiwa kufanyiwa vipimo kadhaa katika Hospitali ya Mulago kwa muda wa miaka mitatu lakini hakukutwa na ugonjwa wowote ndipo alipoamua kwenda kanisani kwa ajili ya kuombewa.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa rafiki zake waliamua kumtafutia msaada wa kiimani na ndipo walimpeleka katika kanisani hapo ambapo umauti ulimkuta.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad