Watu 12 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 50 wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Frester lililokuwa likitoka Bukoba kwenda Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na Lori lenye shehena ya saruji
Ajali hiyo imetokea saa sita usiku wa kuamkia leo Februari 9, 2023 katika Kijiji Cha Silwa Pandambili barabara kuu ya Dodoma - Morogoro huku chanzo cha ajali hiyo ikidaiwa ni dereva wa basi kutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari