AKA Hakupigwa Risasi Tano Kama Ilivyotangazwa, Video Yaonesha ni Risasi Moja tu iliondoa Uhai


Nimeiangalia video kwa umakini mkubwa, inaonekana AKA kapigwa Risasi moja tu, ya kichwa

Hizi taarifa za Risasi tano na nyinginezo zinanichanga sana

Iko hivi, aliyemuua AKA ametokea upande wa nyuma (kulia kwake) na amempiga Risasi ya kichwa, na AKA hakuwa na kauli tena zaidi ya hapo kilichofuata ni kuanguka

Nadhani, Mashuhuda walihesabu risasi zilizopigwa bila kuona zinamlenga nani maana upande wa pili kulikuwa na mtu mwingine akipiga risasi tofauti na huyo aliyempiga AKA.

Na inaonekana walioumia kwenye shambulio hilo walipigwa na mtu mwingine tofauti na aliyempiga AKA. Labda kama Camera zinadanganya, ila kwa risasi sita nitakataa hadi kesho🔨

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad