Buchosa. Mtu moja aliyetambulika kwa jina la Musa Robert anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 76 mkazi wa Kijiji cha Kasheka kata ya Bangwe Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza amekutwa amefariki dunia pembezoni mwa ziwa Victoria katika kitongoji cha Kisenya Kijiji cha Katwe kata ya Katwe wilayani humo huku sehemu zake za siri zikiwa zimenyofolewa.
Ofisa mtendaji Kijiji cha Katwe, Ezekiery Galula akizungumuza na Mwananchi February 12, 2023 amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limeleta simanzi kwa wananchi wa maeneo hayo.
Amesema alipata taarifa kutoka la raia wema waliopita maeneo hayo wakiwa wanakwenda kufanya shughuli za kujipatia kipato ndipo walipoona mwili huo na kutoa taarifa.
Mdogo wa marehemu Manyindo Robert (74) amesema kaka yake alikuwa anatoka nyumbani kwao Kijiji cha Kasheka akielekea Kijiji cha Katwe Kitongoji cha Kisenya kusalimia ndugu na jamaa alipokaribia maeneo hayo alisikia wananchi wakipiga yowe kama ilivyo miLa na desturi aliungana na wananchi wa maeneo hayo hadi sehemu ya tukio na alipofika alimutambua kuwa aliyefariki kuwa na kaka yake.
Manyindo amesema sehemu za siri kwenye mwili wa marehumu kaka yake zilikuwa zimenyofolewa na hazijulikani zilipo licha na viungo vingine kuwepo.
"Kitu kilichonitambulisha ni vidole vyake, kichwa sambamba na nundu aliyokuwa nayo mgongoni, kilichoondoa uhai wake hata mimi sikuelewi mwili huu umesafirisha hadi nyumbani kwake Kijiji cha Kasheka kwa ajili ya maziko, marehemu ameacha mke na watoto wanane.” amesema Manyindo.
Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Katwe, Alizabert John amesema tukio hili limeleta simanzi na sintofahamu kwa jamii hivyo ameviomba vyombo vya usalama kusaidia jambo uchunguzi wa jambo hili.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Katwe, Emmanuel Luzuga amesema mwili huo umepatikana Jana February 11, 2023 majira ya tano asubuhi, pia amewaasa wananchi wasiwe wasisite kutoa taarifa kwa viongozi kwa jambo lolote litakalokuwa halipo sawa.
"Tukio hili linaonekana wazi limetokea kati ya saa nne au tano na wananchi wanapita hapa kwenda kufanya shughuli zao huenda walikuwa wanaogopa kutoa taarifa, tunatakiwa kuwa huru kutoa taarifa.” Amesema Luzuga.
Luzuga amesema jeshi polisi lilifika eneo la tukio kwa ajili ya zoezi la uchunguzi wa tukio hilo ambapo wananchi waliaswa kuwa watulivu wakati vyombo vya usalama vikifanya uchunguzi.