Alhad ampa neno Sheikh mteule Dar, kukabidhi ofisi kesho



Dar es Salaam. Aliyekuwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amewataka Waislamu kumpa ushirikiano Kaimu Sheikh wa mkoa huo Walidi Omar ikiwa ni siku tatu tangu alipoondolewa kwenye nafasi hiyo.

Februari 2, mwaka huu Katibu wa Baraza hilo, Hassan Chizenga akieleza kuwa uwamuzi huo umefanyika baada ya kikao cha Baraza la Ulamaa kilichofanyika kwa siku mbili chini ya Mwenyekiti Mufti Abubakar Zubeir.

Alhad ametoa wito huo huku baraza hilo likimtaka kukabidhi akabidhi ofisi kwa kwa Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salam, Sheik Walidi Februari 7.

Sheikh Alhad amesikika kwenye moja video akisema, Sheikh Walidi anayechukua nafasi yake apewe ushirikiano wa kutosha, kwani rafiki yake na kaka yake na wakisiju mwenziye hivyo apewe ushirikiano wa kutosha.


  “Ntaangalia kesho au keshokutwa nitamkabidhi rasmi ofisi, kama Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, naye tumsaidie maana jiji lina mambo hili, tumsaidie naye katika kiti hiki Mwenyezi Mungu amuongoze na nyie kama Baraza la Masheikh mumsaidie,” amesema.

  “Hizi redio za mbao na mambo na maneno mengine ndio tuko mjini, kila mtu atasema hili na mwenye njaa ataonekana sasa aliyeshiba ataonekana sasa, nyie kama viongozi msaidieni Sheikh Walidi katika nafasi yake hii, msaidieni Mufti fanyeni kazi za baraza na Bakwata kama kawaida,”amesema Sheikh Alhad.

Aidha amewataka kukisaidia chombo hicho ili Waislamu waendelee kubaki na umoja wao kwa kuwa brabra nyingine ni watu wako mjini wanajua namna gani wanatafuta maisha hivyo wao waendelee kuwa wamoja.


Uwamuzi wa kumtengua Sheikh Alhad ulikuja baada ya kiongozi huyo kutangaza kuivunja ndoa ya mtaalamu wa tiba mbadala, Juma Mwaka na mkewe Queen Masanja Januari 25 mwaka huu kutokana na ombi la mwanamke huyo kudai talaka.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad