Aliyefukiwa na Kifusi kwa Siku 11 Akutwa Hai

 


Waokoaji nchini Uturuki wamefanikiwa kumtoa kijana mdogo akiwa hai kutoka kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka ikiwa ni siku 11 baada ya tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.8 kwa kipimo cha rikta lililotokea kusini mashariki mwa Uturuki na Syria.


Kijana huyo, Osman Halebiye (14), aliokolewa na kupelekwa Hospitali huko Antakya ambapo pia baadaye wanaume wawili, Mehmet Ali Sakiroglu (26) na Mustafa Avci (33), waliokolewa kutoka vifusi vya jengo hilo.


Zaidi ya watu 43,000 nchini Uturuki na Syria wamefariki kutokana na tetemeko la ardhi na maelfu wamekoseshwa makazi huku nchi mbalimbali zikijitokeza kutoa msaada wa uokozi, vifaa, chakula na mablanketi kutokana na eneo hilo kuwa na baridi kali.


Tayari Umoja wa Mataifa – UN, umetoa wito wa kuchangishwa zaidi ya dola bilioni moja kushughulikia operesheni za kiutu nchini Uturuki, ikiwa ni siku mbili kupita baada ya kutoa ombi la dola milioni 400 kwa ajili ya watu wa Syria.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad