Amapiano za Tanzania Hazitambuliki Afrika Kusini? Au ni Fitina?


Katika moja ya habari kubwa ya kiburudani ambayo imesambaa sana mitandaoi ni hii ya Tuzo za Amapiano ambapo majina ya wasanii kutoka Afrika Kusini wanaowania Tuzo hizi pamoja na majina ya wasanii wa nje ya Afrika Kusini kwenye kipengele cha 'Friends of Amapiano' kutolewa kwa wasanii kuwani tuzo hiyo hivi leo.


Kutokana na muziki huu kuwaa maarufu Duniani na kwa bara la Afrika muziki huo kufanywa zaidi katika mataifa ya Afrika Kusini, Nigeria na Tanzania.


Katika kitu ambacho wengi wameshangazwa ni baada ya kuona wasanii kutoka Tanzania waliofanya muziki huu kutotajwa kwenye tuzo hizo lakini pia kukosekana kwa wimbo au jina la msanii kutoka Tanzania au Afrika Mashariki licha ya muziki huo kufanywa zaidi nchini Tanzania.

-

Kwenye Vipengele ambavyo palitegemewa kuwa na msanii kutoka Tanzania kuwepo na badala yake wasanii 4 kutoka Nigeria na wengine kutoka Afrika Kusini ndio wamejazana kwenye kipengele hizo.


Friends of Amapiano

Ami Faku - Afrika Kusini

*Asake - Nigeria

Beast - Afrika Kuisini

Cassper Nyovest- Afrika Kusini

*Davido- NNigeria

Dladla Mshunqisi - Afrika Kusini

Mac Gee - Afrika Kusini

Msaki - Afrika Kusini

Vetkuk & Mahoota - Afrika Kusini

*WizKid - Nigeria.

-

Most Viral Amapiano Song Of the Year

“Ameno Amapiano Remix (You Wanna Bamba)” by Goya Menor & Nektunez


Kwa wasanii hawa inaonyesha ni kwa namna gani muziki wetu haufuatiliwi Afrika Kusini?? nyimbo za wasannii wa Tanzania hazijafanya vizuri mbali ya kushirikisha wasanii kutoka Afrika Kusini??


Unahisi kwanini nyimbo kutoka Tanzania hazikuwepo?? hazikustahili?? unahisi nyimbo gani za Amapiano kutoka Tanzania zilistahili kuwepo kwenye tuzo hizo??


Taja ngoma tano za Amapiano ambazo unahisi zimefanya vizuri zaidi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad