Asagwile Mwasongwe Mshindi wa Bongo Star Search - BSS 2023

 

Asagwile Mwasongwe Mshindi wa Bongo Star Search - BSS 2023

Hatimaye Mshindi wa BSS 2023 kwenye msimu wa 13 ametangazwa usiku huu Jijini Dar es salaam kuwa ni Asagwile Mwasongwe huku mshindi wa pili akitangazwa kuwa ni Leonard Sanga na wa tatu akiwa ni Patrick Alsina.


Mshindi wa kwanza amezawadiwa shilingi milioni 20, Mahindi wa pili shilingi milioni 3 huku Mshindi wa tatu akichukua milioni 1.


“Siamini kama nimeshinda, joto lilikuwa kubwa tofauti na BSS ya mwaka 2018. Mwaka huu washiriki wote walikuwa wakali. Patrick, Leonard wote wazuri. Hata nilipoingia mbili bora na Leonard niliamini siwezi kutoboa kwa sababu mwenzangu alikuwa anaongoza hata kwa kura.


"Furaha yangu haielezeki, niliahidi nitatoa kwa Mungu wangu hivyo lazima nitekeleze, kisha kiasi kitakachobakk nitawekeza kwenye muziki wangu kuuendeleza,” alisema Asagwile.


Mgeni rasmi ambaye ni Waziri Wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa amechangia milioni 7 kwenye mashindano hayo;


“Mimi kama mimi nitachangia Milioni 7 na kuahidi kuwasajili bure na kuwapa vyeti vya kutambuliwa na BASATA Washindi hao wote kwenye tatu bora.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad