Azam Ltd yakanusha Taarifa Juu ya Bidhaa yake kutokua salama


Uongozi wa Kampuni ya BAKHRESA FOOD PRODUCTS LTD umekanusha taarifa ambayo inasambazwa katika mitandao ya kijamii, kuwa bidhaa ya kampuni hiyo ya AZAM EMBE si salama kwa walaji na haitengenezwi kutokana na Juisi halisi ya Embe. Pia matumizi ya kiambatanishi (Food Additive) cha Sodium Benzoate kilichowekwa katika kinywaji hicho kinaweza kusababisha madhara ya kiafya kwa walaji.

“Tunakanusha vikali taarifa hizi zinazosambaa kuwa si sahihi. Bidhaa hii inatengenezwa na juisi halisi ya embe na imethibitishwa na mamlaka husika. Matumizi ya kiambatanishi (Food additives) Sodium Benzoate ni ya kawaida kwa aina ya bidhaa hii. Benzoate ni aina ya chumvi inayosaidia bidhaa ikae kwa muda mrefu bila kuharibika. Kiambatanishi hiki ni salama na kimeidhinishwa na mamlaka zinazosimamia uzalishaji wa chakula hapa nchini kuwa ni salama na kinaruhusiwa kutumika katika bidhaa za chakula. Taarifa hizi zinazosambazwa hazina ukweli wowote na zimelenga kupotosha ukweli na kuichafua kampuni.” Imesema taarifa ya uongozi wa kampuni hiyo.

“Tunapenda kuchukua nafasi hii kuwahakikishia wateja wetu kuwa kampuni yetu itaendelea kuzalisha bidhaa bora zenye viwango na kuzingatia usalama wa wateja wetu.” imesema Taarifa hiyo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad