Babu Tale "Nashukuru Bunge Kutumia Dakika 45 Kujadili Udaktari Wangu"


Bado Mbunge wa Morogoro kusini Mashariki, Hamis Taletale almaarufu Dr. @babutale ameendelea kushikilia channel kuhusiana na Udaktari wake wa Heshima aliotunukiwa hivi karibuni na moja ya chuo tokea nchini Marekani, kuwa anastahili kuwa na heshima hiyo kwa kile alicho kifanya kwenye sanaa ya Muziki nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka 27 tangu aingie rasmi upande huo.


Akiiambia Ayo Tv, Babu Tale ameeleza kuwa amefanya kazi kubwa kukitengeneza kiwanda hiki, amesaidia wengi ambao wengine hata wasiposema, wamepita kwenye mikono yake, ni moja ya watu wachache ambao wapo tangu muziki upo kwenye transition ya kutoka kuwa Kipaji hadi kuwa biashara.


Lakini pia Mbunge huyo na Moja ya Mameneja wakuu watatu wa #wcb ameshukuru Bunge kutumia dakika 45 kujadili udaktari wake. Tale amesema hajapew Udokta kwaajili ya Ubunge bali kwa kile alichoifanyia jamii kupitia Muziki.


Hili limekuja baada ya hii leo Feb 09,2023 Mbunge wa jimbo la Mlalo, Rashid Shangazi kusimama Bungeni na kutaka Muongozo kutoka kwa Waziri wa Elimu kama Vyuo vinavyotoa Degree za Heshima vinatambulika na Wizara inayo husika na usimamizi wa Elimu nchini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad