Balozi wa Tanzania Nchini Uturuki "Watanzania Wapo Salama"


Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Luteni Jenerali Mstaafu Yacoub Mohamed amewataka Watanzania walio na ndugu zao nchini Uturuki kufanya mawasiliano kujua hali zao kisha kutoa taarifa endapo kuna madhara ili waweze kuchukua hatua, baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi lililosababisha vifo zaidi ya watu 1,000 nchini humo.

Balozi Mohamed ameyasema hayo hii leo Februari 7, 2023 wakati akifanya mahojiano na Mwandishi wa shirika la Utangazaji nchini – TBC na kusema hadi kufikia sasa kwa Watanzania waliowasiliana nao hali zao ni shwari na kwamba kama kuna yeyote ambaye ana taarifa za ziada anatakiwa kuziwasilisha ili zifanyiwe kazi.

Tukio hilo la tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.8 kwa kipimo cha richa, ambalo limezikumba nchi za Uturuki na Syria limesababisha majeruhi na vifo vingi, ambapo idadi ya waliofariki inaendelea kuongezeka.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad