Breaking News: Rais Samia Apangua Mawaziri Hawa..Yumo Mchengerwa


Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ambapo amemuhamishia Mohamed Omary Mchengerwa aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii huku Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii akihamishiwa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo.

Rais Samia pia amemuhamishia Dkt. Hassan Abbas Said, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii akichukua anachukua nafasi ya Profesa Eliamani M. Sedoyeka.

Rais Samia pia amemteua Said Othman Yakub kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo akichukua nafasi ya Dkt. Hassan Abbas Said, Kabla ya uteuzi huo, Yakub alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. #MillardAyoUPDATES

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad