CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemtaka Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, kujiuzulu wadhifa wake ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za malipo ya baadhi ya miradi nje ya bajeti. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Wito huo umetolewa leo tarehe 7 Februari 2023 na Mjumbe wa Bunge la Wananchi la Chadema, Ahobokile Mwaitenda, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Mwigulu na wote waliohusiska na malipo nje ya bajeti wapishe uchunguzi huru wa kilichofanyika kwenye matumizi nje ya bajeti bila ruhusa ya bunge na kuvunja sheria mbili za wizara ya fedha,” amedai Mwaikenda.
Mwaikenda ametaja baadhi ya maeneo ambayo amedai fedha zake zilitolewa nje ya bajeti ikiwemo ununuzi wa mbolea uliogharimu Sh. 86 bilioni, pamoja na malipo ya kiasi cha Sh. 350 bilioni yaliyofanywa na Serikali katika Kampuni ya Symbion, kama fidia ya kuvunja mkataba kinyume cha sheria.
Katika hatua nyingine, Mwaikenda amedai kuna ubadhirifu katika mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), kipande cha kutoka Tabora hadi Kigoma, akidai mkataba wa ujenzi wa kipande hicho ulikiuka sheria za nchi kwa kuwa mkandarasi alipatikana bila ushindani.
“Upatikanaji wa mkandarasi kwa singlesource limit (bila ushindani)zake zikoje ? Imekuaje mradi wa SGR kutoka Tabora –Kigoma iingie mkataba lot 6 wa km 506 , kwa Sh. 6.34 trilion , wakati hapo hapo ilikuwa na mkataba Isaka –Mwanza wa km 341 wa Sh. 3.12 trillion. Gharama za Isaka -Mwanza ni Sh. 9.1 billion wakatii Sh. 12.5 billion kwa kilomita,” amedai Mwaikenda.
Mwanahalisi