Chris Brown Achefukwa Vibaya, Awatolea Povu zito Waandaji Tuzo za Grammy

Chris Brown achefukwa, awatolea povu zito waandaji tuzo za Grammy


Mwanamuzi nyota wa R&B kutoka nchini Marekani Chris Brown ameshindwa kujizuia baada ya kutopata tuzo ya Grammy katika kipengele kilichomuhusisha, kikizishindanisha album bora za R&B kwa mwaka 2022, ambapo tuzo hiyo imeenda kwa mwimbaji Robert Glasper.


Breezy ameshindwa kujizuia na kuvunja ukimya kutokana na matokeo hayo na kuamua kuutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram (Insta story) kuweka wazi kotoridhishwa na na suala hilo, ambapo amechapisha picha ya ushindi wa Glasper na kuandika maneno yenye kusomeka “Yalll playing,” akimaanisha ‘mnacheza ninyi’ huku akiambatanisha na emoji za kucheka. “Huyu ni nani?” Aliuliza Breezy.


Katika post hiyo, Chris ametafsiriwa kama mwenye kuwapiga kijembe Grammy kutokana na kuamini kuwa album yake ilipaswa kuchukua tuzo hiyo na kwamba mwimbaji Glasper hakupaswa kupewa tuzo hiyo kutokana na kutoamini katika uwezo wake na kwamba hata yeye hamjui msanii huyo.


Glasper ni mpiga piano, mtayarishaji, muandishi na mwimbaji ambaye ameshinda Tuzo hiyo ya Grammy katika kipengele cha Albamu Bora ya R&B kupitia album yake iitwayo ‘Black Radio III’, ambapo alikuwa akichuana na album za wakali wengine kadhaa ikiwamo Breezy ya Chirs Brown (Deluxe), Good Morning Gorgeous ya Mary J. Blige (Deluxe), Candydrip ya Lucky Daye, na Watch the Sun ya PJ Morton.


Katika historia ya muziki, mwimbaji Glasper amefanikiwa kuingia katika vinyang’anyiro vya tuzo za Grammy mara 12, na kufanikiwa kushinda takriban mara tano, Mwaka 2013 aakiwa na albamu bora ya R&B ya Black Radio, Mwaka 2015 Best Traditionali R&B – Performance for Jesus Children, 2017 Best Compilation Soundtrack, 2021 Best R&B Song for “Better Than I Imagined. Best R&B Album 2023.


Kwa upande mwingine mwimbaji Chris Brown yeye amefanikiwa kuingina kwenye vinyang’anyiro takriban 21 na kufanikiwa kushinda mara moja pekee kupitia album yake F.A.M.E mnamo mwaka 2021

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad