Dereva Huyu Kukamatwa na Kunyang'anywa Leseni

 


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Jumanne Sagini, ameagiza kukamatwa na kunyang'anywa leseni dereva aliyeonekana kwenye video iliyosambaa mitandaoni akikaidi baada ya kusimamishwa na askari wa usalama barabarani na badala yake aliendelea kuendesha gari huku akipiga honi.


Naibu Waziri Sagini ametoa kauli hiyo huku akiagiza wataalamu wa afya kuhakikisha wanawapima afya ya akili madereva.


"Nimeona clip ya dereva wa gari ndogo Trafiki wangu anamsimamisha yeye anampelekea gari, hivi huyo bado yuko barabarani?, akamatwe apelekwe kwenye vyombo vya dola, na leseni yetu anyang'anywe, wakati mwingine Trafiki akikuzuia anataka kukuokoa, mimi nina wasiwasi na akili za madereva wetu," amesema Naibu Waziri Sagini

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad