Kanumba na Ray Kigosi walivuma saana kwenye bongo movie, sio kwa sababu walikuwa bora saana ila ushindani uliokwepo, Mwenyezi Mungu alipo mchukua Kanumba mbele za haki, Ray Kigosi I think ametafuta shughuli nyingine ya kufanya.
Nasma Hamis Kidogo Vs Hadija Kopa, kwa wale wahenga kidogo wanajua jinsi wababe hawa wa taarabu walivyokuwa kuwa juu lakini Najma alivyoenda mbele za haki Kopa tunamuona tu kwenye matamasha ya Zuchu tumesahau hata kama naye ni Mwanamuziki.
Ray C Vs Komando Jide , Ray C alipopata changamoto na kupotea kwenye music hata Lady Jay dee kwa sasa anazidiwa mpaka na mabinti wa juzi licha ya kuwa Jay dee nyimbo zake zina ujumbe, zinaishi, zinaelimisha kuliko hawa mabinti wanaoimba za kwikwi jogoo anawika.
Ally Choki na Banza Stone, hii miamba ina historia kubwa kwenye music wa dansi wa kisasa, lakini baada ya Banza stone kutangulia mbele za haki, kwa mara ya mwisho nilisikia Ally Choki amekuwa MC ametafuta.
Uwepo wa Simba Imara ndio kunafanya Yanga ifanye vizuri zaidi.
Vitu viwili vinavyovyutana sio kwa ubaya ila kwa kuendeleza kitu fulani ni jambo jema, ushindani huleta ubunifu na jitihada za kufanya vizuri.
Diamond endelea kumombea sana Harmonize aendeleee kuwepo kwenye game, Tanzania yote inajua hakuna unachodaiwa kwenye bongo fleva lakini ukweli mchungu ni kuwa nyimbo zako sio za kuishi, nyimbo za chutama mkongojo upite ni nyimbo zinazodumu kwa siku chache, upinzani wako na Harmonize kwa sasa unakufanya uwe juu zaidi kimuziki na Harmonize bila wewe kuwa juu naye jioni tu atakuwa amesahaulika maana nyimbo za koh koh sio za kuishi.
Sio kwa ubaya kwa soko la sasa linahitaji nyimbo hizo mnazoimba, Music umekuwa Biashara kubwa hivyo ni lazima uzalishe product inayotakiwa na wateja..
Ni muhimu saana wakati unaombea familia yako USISAHAU KUMUOMBEA ADUI YAKO MAANA KUNA NAMNA ANAFANYA AU ANAMCHANGO WA WEWE KUWEPO HAPO ULIPO YAWEZEKANA HATA BILA YEYE KUJUA.