Diva Awapokea Watoto Watano wa Mumewe Aliozaa na Wanawake Tofauti

 


Mtangazaji wa kituo cha redio cha Wasafi FM, Diva The Bawse amefichua jinsi alivyoolewa na mumewe, bila kujua kwamba jamaa alikuwa na watoto.


Diva ambaye mtangazaji wa kipindi cha Lavidavi cha Wasafi FM, alisema watoto hao walianza kuonekana baada yao kufunga ndoa rasmi.


Akizungumza na kituo kimoja cha redio, Diva alisema kuwa mumewe alizaa karibu watoto watano na wanawake wengine.


“Baada ya kuoana, mwanamke mmoja alimpigia simu akimwambia kwamba mumewe alikuwa baba wa mtoto wake wa miaka mitatu. Hawakuwa kwenye uhusiano alipopata ujauzito. Hapo awali hakuwa na uhakika kama mtoto huyo alikuwa wake."


Diva alifichua kuwa mume wake aliogopa kumpa taarifa kuhusu mtoto huyo lakini baadaye akafanya hivyo.


"Alinitumia picha za mtoto huyo mtanashati. Nilimwambia tunaweza kuishi na mtoto huyo ikiwa mamake hana tatizo.”


Kulingana na Diva, idadi ya watoto ambao mumewe iliongezeka hadi watano, lakini kuna uwezekano ni wengi zaidi ya hapo.


“Hadi sasa, tumethibitisha watoto watano kuwa wake. Wananiita shangazi Diva.”


Hata hivyo, Diva alisema hana kinyongo cha kukaa na watoto hao.


“Hata wakilea watoto kumi, nitawalea wote ilimradi tu mume wangu awajukumikie mahitaji yao. Watoto ni baraka.”


Mwanahabari huyo alibainisha kuwa alilelewa na ndugu zake wa kambo, na walipendana sana.


“Ndugu zangu wawili wanatoka kwa mama tofauti, lakini huwezi kujua. Tumeishi kwa amani na kupendana."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad