Familia ya marehemu ‘AKA’ yarudi na tamko hili jipya

 




Familia ya rapper AKA imetoa taarifa rasmi ya ratiba inayoelezea taratibu za mazishi ya nyota huyo aliyefariki kwa kupigwa risasi mwishoni mwa juma lililopita huko Durban nchini Afrika kusini.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mazishi ya nyota huyo yamepangwa kufanyika siku ya Jumamosi Februari 18, 2023, yakihusisha ndugu na watu wa karibu wa familia pekee.


Huku mashabiki wakitangaziwa kutazama tukio hilo kupitia matangazo ya moja kwa moja kwenye YouTube channel ya marehemu ‘AKA” mwenyewe.


 

“Sisi kama familia ya Forbes tungependa kukiri heshima na upendo mkubwa ambao tumeupokea katika siku chache zilizopita. Kiernan hakupendwa tu na sisi kama familia bali na taifa zima.


Kiernan ‘AKA’ atazikwa katika mazishi ya kibinafsi Jumamosi, Februari ya 18, 2023, ibada ya ukumbumbusho itafanyika Ijumaa, Februari 17, 2023 katika Kituo cha mikutano cha Sandton.


Wale wanaotaka kuhudhuria wanaweza kufanya hivyo kwa kujipatia tiketi kwenye tovuti Ya Webticket. Ibada ya ukumbusho wake pia itaruka mubashara kwenye Youtube chaneli ya AKA duniani kote” Imesema taarifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad