Gari la Abiria Latumbukia Kwenye Korongo, Majeruhi na Kifo Charipotiwa



Mtu mmoja (Dereva) amefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa katika Kata ya Sigino Wilayani Babati Mkoani Manyara baada ya gari la abiria (Coaster) kufeli breki na kutumbukia korongoni.

Akiongea kwa njia ya simu RPC wa Manyara, George Katabazi amesema gari hilo lilikuwa linatokea Mkoani Singida kuelekea Arusha na baada ya kufika eneo la kona ya Logia ndipo likafeli breki na kumshinda Dereva.


“Ajali imetokea leo, gari lilikuwa na Watu 29 abiria ni 27 Dereva mmoja pamoja na utingo wake, Dereva amefariki huku majeruhi wakiwa saba ambapo kati yao watatu hali zao ni mbaya ila abiria wengine walipata mshtuko tu, chanzo cha ajali ni kufeli kwa mfumo wa breki wa gari hali iliyopelekea kumshinda Dereva kulimudu gari hilo na kuingia kwenye korongo”




Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad