Harmonize ameendelea kukazia juu ya sakata lake la madai aliloliweka wazi wiki iliyopita mtandaoni kwamba hajawahi kufaidika na mauzo ya kazi zake na kudai kuna watu wamekuwa wakichukua pesa katika platforms zilipo nyimbo zake.
Konde amezitaja Wasafi pamoja na Kampuni ya Mziiki na kusema anahitaji wanasheria 5 ili kuweza kudili na suala hilo, akisema kampuni hizo zimeungana kuchezea maisha yake licha ya kutowafanyia baya lolote.
"Ubaya unaanza pale mtu unapotaka jasho lako ili usaidie familia yako kama wao wanavyofanya..." - Ameeleza.
Aidha, boss huyo wa Konde Gang, amemuomba Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA aanze na hilo jambo lake ili kuweza kupata haki yake inayozidi kupotea.
"Kaka mkubwa hongera na nakuomba uanze na hili. Mama anajua kabisa wewe ni SULUHU nyengine..." Ameeleza.
Pia kwenye ujumbe wake huo mrefu kupitia insta story yake amebainisha kwamba, kwa miaka mitatu sasa hajawahi kukusanya mapato yake ya Publishing (pesa zinazotokana na mauzo ya muziki wake) kutoka vyanzo mbalimbali lakini hivi karibuni alipata simu toka kampuni ya Ziiki akaambiwa kuna kiasi cha Sh. Milioni 58 pekee.