Harmonize Ajipa Likizo ya Mapenzi



Msanii wa Bongo Fleva toka Konde Music Worldwide, Harmonize amesema kutokana na kupitia mengi ya kuumizwa katika mahusiano, sasa amejipa mapumziko.


Katika taarifa aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram siku ya Jumatano, Harmonize amesema kwamba kwa sasa anajipatia muda usiojulikana wa mapumziko kabla ya kujitosa kwenye mahusiano mapya.


“Msijali, hivi karibuni nitapata mtu na mtamjua!!,” alisema.


Staa huyo alidokeza kwamba alipitia masaibu mengi mno wakati akiwa katika mahusiano yake ya awali. “Wasikuone na kidem tuu!! Hivi mnajua niliyo yapitia,” aliandika.


Utakumbuka Kajala Masanja alithibitisha kutengana na Harmonize mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuchumbiana naye kwa takriban miezi saba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad