Harmonize "Kina REMA, RUGER na OMALAY Wanalipwa Mkwanja Mrefu Kuliko Sisi East Afrika"

 


''Asanteni Kwa Mapokezi Makubwa Ya #SA❤️‍🩹 Huu Wimbo Hata Msinge Uthamini Na Kuupa Nafasi Kama ilivyo Now Pengine Isingeniumiza Nachukulia Kama Mwanzo Wa Safari Yangu Ya kuzikimbilia Ndoto Imekuwa Ni Ndoto Ya kila Msanii Kufanya Matamasha Makubwa Na kujaza Watu Wengi Kama Wenzetu Tunaolinganishwa nao Wa West Africa Hadi kupelekea Tunatukanwa Tukifanya Show na Kupata Mashabiki Wa Chache Nchi Zanje Ya Africa Ukweli Mchungu Nikwamba Sisi Africa Mashariki Tupo wachache ingawa Tunapendana Sana kulinganisha na Wenzetu West !!! Lakini wachache Hao Hao Karibia Nusu Wanaongea Kizungu Na inakuwa Rahisi Kuzipenda Na Kuziimba Nyimbo Za wenzetu wao Ni Wengi Na pamoja na Uwingi Wao Hata Robo Hawajuwi Tunacho Kiongea Na Kukiimba Tatizo Huanzia Hapo!!!! Ningumu Pia Wimbo Usipo Hit Nyumbani Kwako kuwa Hit Kwa Wenzio!!!!!! Ushauri Wangu TUIPENDE LUGHA yetu Tujivunie Tuiimbe Na Kuipamba Maaana LUGHA Yetu Ndio Fahari Yetu Ndio UTAMADUNI WETU ila Isifikie Pahala Tukazani Mataifa Yote Yanaelewa Hii LUGHA YETU ADHIM!!!! 🙏 nadra Sanaa Kutokea Wimbo Ukawa Maarufu Mataifa amengine inatokea Mara Chache tena NI Pale PRODUCER Akipiga Mdundo Mkali Na Sio Maneno NAIPONGEZA SANA BASATA Kwajitihada Za Kutafuta MDUNDO WA TAIFA penginepo Nasisi Tukapata SOUND YA KUTUTAMBURISHA Kama Ilivyo kwa Wenzetu SOUTH AFRICA Good @basata.tanzania 👏🏻 Tuimbeni tujivuni Tamaduni Zetu Ila tukipata Nafasi Tuwe Tunaimba Hii LUGHA mara Moja Moja Sio Mbaya Ninaimani Itasaidia Kutangaza Tamadini zetu Na Kupelekea Hata Mataifa mengine Kuufwatilia Muziki Wetu Na Kujifunza Hata LUGHA Zetu Pamoja Na Tamaduni Zutu!! Maana Nyimbo Za Namna Hiii Zitawapa Mwangaza Wakujua Tunavipaji Kiasi Gani SHUKRANI SANA WOTE MNAO SUPPORT NYIMBO ZA HIVI PAMOJA NA NYIMBO ZINGINE NA WASIO SUPPORT BASI WASIJIULIZE KWANINI HATUENDI International 🤫 Muache Pia Kutushindanisha Na Wakina Burnaboy & Davido Wizkid Kwasababu Wanasikilizwa Na Kueleweka Wanacho Kiongea Kalibia Na Dunia Nzima!!! 🙏 thank me Later REMA & RUGER OMARAY wametupita Mbali Lol wanalipywa Pesa Nyingi Show Kuliko Msanii Yeyote Wa Africa Mashariki Maana Wanasikilizwa Eneo Kubwa !!!! Sijachelewa HELLOW HELLOW !!! DJS issa Friday Support this SAVE THE GAME'' @harmonize_tz

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad