Harmonize "Tuache CHUKI Zisizo na Maana"


Mwanamuziki @harmonize_tz ametoa kile kilichopo ndani ya moyo wake juu ya mwenendo wa wasanii wa muziki wa Bongofleva kutokuwa na ushirikiano hasa kupeana support ili kukuza muziki wa Bongofleva Kimataifa.


Boss huyo wa Konde Gang ameeleza kuwa, moja ya kitu kinachopelekea muziki wetu kutokuwa mkubwa ni chuki zisizo na maana miongoni mwa wasanii.


"Tunasikilizwa Afrika Mashariki pekee, ndipo tunapoelewaka" - ameeleza @harmonize_tz kwenye sehemu ya ujumbe wake kupitia insta story.


Pia ametolea mfano wanamuziki wa Nigeria akisema wanawachora tu wasanii wa Bongo walivyokuwa hawapendani, wao wako busy ndio maana hawagombani. Wasanii wa Bongofleva wanapishana humu humu ndio maana wanarushiana maneno.


Amebainisha kwamba chuki zitaisha ama kupungua ikiwa msanii una stress za kuujaza O2 Arena (London) siku 3.


"Kiuhalisia tunapendana sana. Sisi ni familia moja, DJ's, wadau, mashabiki na wasanii" - Amemalizia @harmonize_tz kwenye ujumbe wake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad