Hatimaye Tundu Lissu Asimulia Hatua kwa Hatua Tukio Zima Mpaka Alivyopigwa Risasi

 

Tundu Lissu asimulia hatua kwa hatua tukio zima mpaka alivyopigwa risas« NyumaMbele »Comments (0) WhatsApp Facebook Twitter Email This Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu. Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu. Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesimulia alivyofuatiliwa hadi kupigwa risasi miaka mitano iliyopita.  Septemba 7, 2017, Lissu, akiwa Mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni kipindi hicho, alishambuliwa kwa kupigwa risasi zaidi ya 38 mjini Dodoma.  Tukio hilo liliripotiwa kutendwa dhidi yake majira ya mchana, akishambuliwa kwa risasi akiwa anajiandaa kushuka kwenye gari lake nyumbani kwake Area D jijini Dodoma baada ya kushiriki mkutano wa asubuhi wa Bunge ambao pia alikuwa miongoni mwa waliochangia hoja.  Baada ya shambulio hilo, Lissu alipelekwa Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Dodoma kupata matibabu ya awali na baadaye alipelekwa Nairobi, Kenya kwa ajili ya matibabu ya kibingwa kisha kuhamishiwa Ubelgiji ambako alitibiwa kwa muda mrefu zaidi na baadaye kuishi huko akihofia kurejea nchini kutokana na kile alichodai kukosa uhakika wa usalama wake.  Katika mahojiano na kituo cha runinga cha Clouds juzi alasiri, Lissu alifunguka kwa undani kuhusu tukio hilo lililotikisa kitaifa na kimataifa, akidai kulikuwa na magari mawili yaliyokuwa yanamfuatilia kuanzia alipotoka bungeni kwenda nyumbani kwa ajili ya kupata chakula cha mchana.  Lissu ambaye ni mtaalamu wa sheria, alisisitiza kuwa kuwapo kwake hai hadi leo ni Mungu tu na wala si utashi wake mwenyewe.  "Septemba 7 (2017), niliondoka nyumbani kwenda Dodoma, kuna eneo linaitwa Area D, kuna maghorofa mengi, ndiko wanakaa viongozi wa serikali na yanalindwa muda wote, nimeishi pale toka mwaka 2010.  "Nilifika bungeni, tukajadili na nilikuwa mtu wa mwisho kuzungumza katika ile session (kikao) ya asubuhi inayoisha saa saba mchana.  "Baada ya kumaliza, nikatoka nje nikampigia dereva wangu simu aje anichukue twende nyumbani tukale chakula cha mchana.  "Mimi siku zote ninakula nyumbani, ninapenda ugali na maziwa, ukiwa bungeni miaka ile njia rahisi ilikuwa inapita katikati ya uwanja wa ndege.  "Sasa siku hiyo ilikuwa imefungwa, sababu palikuwa panafanyiwa matengenezo. Kwa hiyo, ili uende Area D, inabidi uende mjini hivyo tukaelekea mjini," Lissu alisimulia.  Mwanasiasa huyo aliyerejea nchini mwezi uliopita baada ya kuwa ughaibuni kwa kipindi kirefu, alisema kuwa walipopita 'round about' ya Singida, wakapita 'round about' ya barabara ya Arusha ambayo inapakana na uwanja wa ndege, dereva wake alimwambia kuna magari mawili yalikuwa yanawafuata nyuma na walikuwa nayo tangu walipotoka mjini.  Lissu aliendelea kusimulia kuwa baada ya dereva wake kumwambia hivyo, alimjibu kwamba "hawa polisi wananifuatilia nini kwa sababu mimi nilikuwa ninasumbuliwa sana na polisi na nikiangalia wiki hii nimekaa kimya sana kwa sababu sijaongea jambo la kuwafanya wakose raha".  Mtaalamu huyo wa sheria aliendelea kusimulia kilichojiri, akitamka: "Tukafika Area C bado tuko nao, magari yalikuwa mawili -- Landcruiser nyeupe na Mitsubishi, tukaenda mpaka Area D tumekaribia getini kama kuna mtu anafahamu iliko Club84, kutoka hapo ni kama mita 20 hadi kufika hapo.  "Tulipopita pale, Landcruiser nyeupe ikapaki pembeni, Mitsubishi ikaja tukaingia nayo mpaka getini.  "Lile geti huwa linafungwa muda wote na huwa kuna walinzi wawili au watatu, lakini siku hiyo geti lilikuwa wazi na hakukuwa na mlinzi, tukapita tukaenda Block E niliyokuwa ninaishi."  Lissu alidai kuwa walipofika eneo hilo, waliingia sehemu ya kupaki gari huku lile gari lililokuwa linawafuatilia likiwa nyuma yao.  "Bahati nzuri siku hiyo magari yalikuwa mengi na nafasi ya kupaki ilikuwa imebaki ndogo yalikuwapo magari mengi ya viongozi wengine, yalikuwa bado hayajatoka. Kwa hiyo, sehemu ya kupaki ilikuwa moja. Kwa sababu sisi tulikuwa mbele, dereva akaiingiza gari kwenye nafasi iliyokuwa imebaki," alidai.  Lissu alidai kuwa dereva aliyekuwa anaendesha gari lililokuwa nyuma yao, alikuwa anatafuta eneo la kupaki na kwa kuwa hapakuwa na nafasi nyingine, alikosa nafasi, akageuza gari kuelekea walikotokea.  "Baada ya kuona hali hiyo, dereva akaniambia nisishuke kwanza nisubiri. Baada ya kuona sishuki kwenye lile gari na wao wakawa wananisubiri.  "Baada ya muda kidogo, mmoja aliyekuwa amekaa siti ya nyuma, akashuka akaenda kuongea mbele upande wa abiria, wakazungumza kidogo akarudi ndani.  "Ninafikiri walikuwa wanajadili 'sasa jamaa hashuki tunafanyaje?' Mimi hapo ninaona mchezo wote kwa kupitia vioo vya kwenye gari.  "Baada ya muda kidogo, yule aliyekuwa ameshuka na yule mwingine akafungua, wakiwa na mashine aina ya SMG (Short Machine Gun), hapo wakaachia.  "Paa! paaa! paaa! Walivyoanza tu, dereva wangu akanivuta upande wake, yeye akaruka akakimbia. Kwenye gari langu kuna friji nikawa nimelilalia na kiwiliwili changu nilikuwa kwenye siti ya dereva walinichakaza sana kwenye eneo la paja na mgongo kidogo.  "Walipomaliza kukawa kimya, ghafla baadaye dada yangu wa kazi, Amina ambaye huwa anatupikia chakula alikuwa anatusubiri twende kula, akaja akaona gari jinsi lilivyochakazwa.  "Na dereva wangu akatoka alikokuwa amejificha, mikono yangu ilikuwa imevunjwa na nimepigwa vibaya.  "Wakaninyanyua wakaniweka sawa kwenye siti. Baada ya hapo, wakanichukua kwa kutumia gari la Naibu Spika, wakanipeleka hospitalini," alisimulia.  Lissu alisema kuwa alimwambia dereva wake awapigie wafuasi wa chama chake kuwajulisha kilichotokea na alipofika hospitalini alimkuta Mwenyekiti (Freeman Mbowe) ameshafika baada ya kupata habari.  Alisema mwanzoni hakuona maumivu yoyote kwa kuwa mwili wake ulikuwa kama umekufa ganzi na baada ya hapo hakuelewa kilichoendelea kwa kuwa alipoteza fahamu na alizinduka akiwa Nairobi.  Hadi sasa hakuna aliyekamatwa na Jeshi la Polisi (lenye mamlaka hayo kisheria) kutokana na tukio la shambulio dhidi ya Lissu.  Lissu amerejea nchini kuendelea na shughuli za kisiasa, akitokea Ubelgiji alikokuwa anaishi. Uamuzi huo umefanyika kwa baraka za chama siku chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuondoa zuio la mikutano ya kisiasa kwa vyama vya siasa lililodumu kwa takribani miaka saba.

Septemba 7, 2017, Lissu, akiwa Mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni kipindi hicho, alishambuliwa kwa kupigwa risasi zaidi ya 38 mjini Dodoma.


Tukio hilo liliripotiwa kutendwa dhidi yake majira ya mchana, akishambuliwa kwa risasi akiwa anajiandaa kushuka kwenye gari lake nyumbani kwake Area D jijini Dodoma baada ya kushiriki mkutano wa asubuhi wa Bunge ambao pia alikuwa miongoni mwa waliochangia hoja.


Baada ya shambulio hilo, Lissu alipelekwa Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Dodoma kupata matibabu ya awali na baadaye alipelekwa Nairobi, Kenya kwa ajili ya matibabu ya kibingwa kisha kuhamishiwa Ubelgiji ambako alitibiwa kwa muda mrefu zaidi na baadaye kuishi huko akihofia kurejea nchini kutokana na kile alichodai kukosa uhakika wa usalama wake.


Katika mahojiano na kituo cha runinga cha Clouds juzi alasiri, Lissu alifunguka kwa undani kuhusu tukio hilo lililotikisa kitaifa na kimataifa, akidai kulikuwa na magari mawili yaliyokuwa yanamfuatilia kuanzia alipotoka bungeni kwenda nyumbani kwa ajili ya kupata chakula cha mchana.


Lissu ambaye ni mtaalamu wa sheria, alisisitiza kuwa kuwapo kwake hai hadi leo ni Mungu tu na wala si utashi wake mwenyewe.


"Septemba 7 (2017), niliondoka nyumbani kwenda Dodoma, kuna eneo linaitwa Area D, kuna maghorofa mengi, ndiko wanakaa viongozi wa serikali na yanalindwa muda wote, nimeishi pale toka mwaka 2010.


"Nilifika bungeni, tukajadili na nilikuwa mtu wa mwisho kuzungumza katika ile session (kikao) ya asubuhi inayoisha saa saba mchana.


"Baada ya kumaliza, nikatoka nje nikampigia dereva wangu simu aje anichukue twende nyumbani tukale chakula cha mchana.


"Mimi siku zote ninakula nyumbani, ninapenda ugali na maziwa, ukiwa bungeni miaka ile njia rahisi ilikuwa inapita katikati ya uwanja wa ndege.


"Sasa siku hiyo ilikuwa imefungwa, sababu palikuwa panafanyiwa matengenezo. Kwa hiyo, ili uende Area D, inabidi uende mjini hivyo tukaelekea mjini," Lissu alisimulia.


Mwanasiasa huyo aliyerejea nchini mwezi uliopita baada ya kuwa ughaibuni kwa kipindi kirefu, alisema kuwa walipopita 'round about' ya Singida, wakapita 'round about' ya barabara ya Arusha ambayo inapakana na uwanja wa ndege, dereva wake alimwambia kuna magari mawili yalikuwa yanawafuata nyuma na walikuwa nayo tangu walipotoka mjini.


Lissu aliendelea kusimulia kuwa baada ya dereva wake kumwambia hivyo, alimjibu kwamba "hawa polisi wananifuatilia nini kwa sababu mimi nilikuwa ninasumbuliwa sana na polisi na nikiangalia wiki hii nimekaa kimya sana kwa sababu sijaongea jambo la kuwafanya wakose raha".


Mtaalamu huyo wa sheria aliendelea kusimulia kilichojiri, akitamka: "Tukafika Area C bado tuko nao, magari yalikuwa mawili -- Landcruiser nyeupe na Mitsubishi, tukaenda mpaka Area D tumekaribia getini kama kuna mtu anafahamu iliko Club84, kutoka hapo ni kama mita 20 hadi kufika hapo.


"Tulipopita pale, Landcruiser nyeupe ikapaki pembeni, Mitsubishi ikaja tukaingia nayo mpaka getini.


"Lile geti huwa linafungwa muda wote na huwa kuna walinzi wawili au watatu, lakini siku hiyo geti lilikuwa wazi na hakukuwa na mlinzi, tukapita tukaenda Block E niliyokuwa ninaishi."


Lissu alidai kuwa walipofika eneo hilo, waliingia sehemu ya kupaki gari huku lile gari lililokuwa linawafuatilia likiwa nyuma yao.


"Bahati nzuri siku hiyo magari yalikuwa mengi na nafasi ya kupaki ilikuwa imebaki ndogo yalikuwapo magari mengi ya viongozi wengine, yalikuwa bado hayajatoka. Kwa hiyo, sehemu ya kupaki ilikuwa moja. Kwa sababu sisi tulikuwa mbele, dereva akaiingiza gari kwenye nafasi iliyokuwa imebaki," alidai.


Lissu alidai kuwa dereva aliyekuwa anaendesha gari lililokuwa nyuma yao, alikuwa anatafuta eneo la kupaki na kwa kuwa hapakuwa na nafasi nyingine, alikosa nafasi, akageuza gari kuelekea walikotokea.


"Baada ya kuona hali hiyo, dereva akaniambia nisishuke kwanza nisubiri. Baada ya kuona sishuki kwenye lile gari na wao wakawa wananisubiri.


"Baada ya muda kidogo, mmoja aliyekuwa amekaa siti ya nyuma, akashuka akaenda kuongea mbele upande wa abiria, wakazungumza kidogo akarudi ndani.


"Ninafikiri walikuwa wanajadili 'sasa jamaa hashuki tunafanyaje?' Mimi hapo ninaona mchezo wote kwa kupitia vioo vya kwenye gari.


"Baada ya muda kidogo, yule aliyekuwa ameshuka na yule mwingine akafungua, wakiwa na mashine aina ya SMG (Short Machine Gun), hapo wakaachia.


"Paa! paaa! paaa! Walivyoanza tu, dereva wangu akanivuta upande wake, yeye akaruka akakimbia. Kwenye gari langu kuna friji nikawa nimelilalia na kiwiliwili changu nilikuwa kwenye siti ya dereva walinichakaza sana kwenye eneo la paja na mgongo kidogo.


"Walipomaliza kukawa kimya, ghafla baadaye dada yangu wa kazi, Amina ambaye huwa anatupikia chakula alikuwa anatusubiri twende kula, akaja akaona gari jinsi lilivyochakazwa.


"Na dereva wangu akatoka alikokuwa amejificha, mikono yangu ilikuwa imevunjwa na nimepigwa vibaya.


"Wakaninyanyua wakaniweka sawa kwenye siti. Baada ya hapo, wakanichukua kwa kutumia gari la Naibu Spika, wakanipeleka hospitalini," alisimulia.


Lissu alisema kuwa alimwambia dereva wake awapigie wafuasi wa chama chake kuwajulisha kilichotokea na alipofika hospitalini alimkuta Mwenyekiti (Freeman Mbowe) ameshafika baada ya kupata habari.


Alisema mwanzoni hakuona maumivu yoyote kwa kuwa mwili wake ulikuwa kama umekufa ganzi na baada ya hapo hakuelewa kilichoendelea kwa kuwa alipoteza fahamu na alizinduka akiwa Nairobi.


Hadi sasa hakuna aliyekamatwa na Jeshi la Polisi (lenye mamlaka hayo kisheria) kutokana na tukio la shambulio dhidi ya Lissu.


Lissu amerejea nchini kuendelea na shughuli za kisiasa, akitokea Ubelgiji alikokuwa anaishi. Uamuzi huo umefanyika kwa baraka za chama siku chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuondoa zuio la mikutano ya kisiasa kwa vyama vya siasa lililodumu kwa takribani miaka saba.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad