Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa DAR



SAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, Sheikh mpya wa mkoa huo Sheikh Walid Alhad Omar amesema ameupokea uteuzi huo na kuahidi kumsaidia Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo tarehe 2 Februari 2023, Sheikh omar amesema anamuomba Mwenyezi Mungu amsaidie kutekeleza majukumu kutokana na uteuzi huo.


Sheikh Omar akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa Baraza la Ulamaa, Sheikh Hassan Said Chizenga
“Nimepokea uteuzi wa Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir…namuomba Mwenyezi Mungu anisaidie kutekeleza uteuzi huu uliokuja, lakini kama inavyojulikana lengo la uteuzi ni kumsaidia katika yale aliyopanga kusaidia jamii ya waislamu wa Tanzania na umma wote kwa ujumla.

“Namuomba Mwenyezi Mungu aniwezeshe kwa fadhila zake kukaimu nafasi hiyo,” amesema Sheikh Omar.

Awali Katibu wa Baraza la Ulamaa, Sheikh Hassan Said Chizenga alitangza Baraza la Ulamaa la Bakwata katika kikao kilichofanyika tarehe 1 Februari 2023 chini Mwenyekiti Mufti Abubakar Zubeir limetengeua uteuzi wa Sheikh Alhad Mussa Salum kama Sheikh wa mkoa Dar es Salaam kuanzia leo tarehe 2 Februari 2023.

Sheikh Chizenga amesema baraza hilo limemteua  Sheikh Walid Alhad Omar kukaimu nafasi hiyo ya Sheikh Alhad Mussa Salum kuanzia leo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad