February 24 mwaka 2019 Lizy Mtango, mtanzania aliyekua akiishi nchini Ujerumani akiugua kansa ya damu kwa muda mrefu (leukemia) alilazimika kuchomwa sindano ya kifo ili apumzike kutokana na mateso ya ugonjwa huo. Silent death (euthanasia) ni utaratibu unaoruhusiwa kwa baadhi ya nchi duniani kwa makubaliano kati ya daktari na mgonjwa mwenyewe. Huduma hii hutolewa kwa wagonjwa walio kwenye maumivu makali na walioteseka kwa muda mrefu na kufikia hatua ya kukata tamaa. Lizy alitumia mtandao wa Whatsapp kuwaaga rafiki zake. Leo ni miaka minne tangu alipotwaliwa katika maisha haya.!
By Malisa GJ