Izzo Business "Mwimbaji Joslin Anahitaji Msaada Mkubwa"


Rapa @izzo_bizness_mbeya ameamua kupaza sauti kwa tasnia ya muziki na jamii kwa ujumla kufuatia video inayomuonesha mwanamuziki Joslin akiwa hayupo kwenye hali nzuri, akisema Joslin anahitaji msaada mapema.

Izzo ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa twitter, “Sema hii inaumiza sana. Moja kati ya vipaji bora kabisa kwenye kiwanda chetu. Joslin anahitaji msaada mapema pasipo kupepesa macho.”

Joslin ambaye ni mkali wa RnB amewahi kutamba na hits kama #NiiteBasi kwasasa ni wazi hayupo kwenye hali nzuri kama ambavyo anaonekana kwenye mahojiano hayo aliyofanyiwa na kipindi cha ICU kinochoongozwa na mtangazaji Kwisa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad