Jeshi la Uganda Limekanusha Kumtesa Mwanaharakati wa Upinzani

 




Jeshi la Uganda limekanusha tuhuma za kumteka nyara na kumtesa mwanaharakati wa upinzani, siku moja baada ya picha kuibuka zikimuonesha mwathiriwa akiwa na alama za mateso zinazoonekana kifuani mwake.


Katika msururu wa jumbe za Twitter, kiongozi wa upinzani Bobi Wine alikuwa amesema mfuasi wake alichomwa na kifaa cha chuma kilichotiwa moto kifuani na vyuma vilitumika kurarua ngozi yake.


“Hii imekuwa hatima ya mamia ya wafuasi wetu wanaotekwa nyara mara kwa mara!”alisema.


Lakini msemaji wa jeshi alisema uchunguzi wa ndani uligundua kuwa mwathiriwa, Eric Mwesigwa, “hakuwa mikononi mwa chombo chochote cha usalama”.


“Tunamshauri aende kwa Tume ya Haki za Kibinadamu ya Uganda (UHRC) na kuripoti au polisi ili tuanze uchunguzi wa kina,” msemaji huyo aliongeza.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad