Kampuni ya Adidas yakiri kujutia kutemana na Kanye West Oktoba mwaka jana kwani kufuatia kitendo hicho, Kampuni hiyo inatarajia kupata hasara ya $1.3 Billioni ambazo ni zaidi ya TSh. Trilioni 3 kwenye mauzo yao kwa mwaka huu.
Kwenye taarifa ya Kampuni hiyo imeeleza kwamba ni kutokana na kushindwa kuuza nguo na viatu vya brand ya "Yeezy" ya rappa Ye ambazo walikuwa tayari wamezizalisha kipindi wapo nae.
Kwa upande mwingine, Adidas imesema inaweza kujaribu kuuza nguo hizo zikiwa zimeondolewa chapa ya "Yeezy" ambapo kama watafanya hivyo basi itawasaidia kuokoa takribani $300 Milioni za kampuni hiyo.
Itakumbukwa, Adidas ilivunja mkataba na Ye Oktoba mwaka 2022 kutokana na matamshi ambayo Kampuni hiyo iliyaita ya chuki dhidi ya Wayahudi.