Serikali nchini Madagasca, imesema Kimbunga chenye nguvu cha kitropiki Freddy, kimesababisha vifo vya watu wanne, idadi ambayo ni ndogo ikilinganishwa na ile ya mwaka jana ambapo Kimbunga cha Batsirai kiliua zaidi ya watu 130.
Ofisi ya Taifa ya Kudhibiti majanga nchini humo, imesema dhoruba hiyo iliathiri takriban watu 16,600 baada ya hayo kupiga na kisha kuelekea nchi za Msumbiji na Zimbabwe.
Mawimbi hayo yenye nguvu ya upepo, yalifikia karibu kilomita 130 kwa saa, na kimekuja tofauti bila kuleta mvua kubwa kama ilivyokuwa mwaka jana kwa kimbunga cha Batsirai ambacho kilileta mvua nyingi.
Freddy ni kimbunga cha kwanza na mfumo wa pili wa hali ya hewa ya kitropiki kuikumba Madagascar katika msimu wa sasa kulingana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA).