KUMEKUCHA Uchaguzi Nigeria: Boko Haram wajeruhi wapiga kura

 

KUMEKUCHA Uchaguzi Nigeria: Boko Haram wajeruhi wapiga kura

Takriban watu watano (wanawake wawili na wanaume watatu), wamejeruhiwa kufuatia watu wanaoshukiwa kuwa ni magaidi wa Boko Haram kufyatua mabomu ya lami toka Milima ya Mandara ya Gwoza, iliyopo eneo la serikali ya mtaa wa Jimbo la Borno wakiwalenga wapiga kura.


Washambuliaji hao, wanahisiwa kutoka kambi ya Ali Ngulde ya kikundi cha Jamā’at Ahl as-Sunnah lid-Da’wah wa’l-Jihad milki ya Boko Haram, na walifanya mashambulizi wakati wapiga kura wakikaribia kuanza mchakato wa upigaji kura wa Rais na Wabunge unaofanyika nchi nzima.


Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka kwa vyanzo vya usalama na Zagazola Makama, Mtaalam wa Kupambana na uasi na Mchambuzi wa Usalama katika Ziwa Chad, amesema mashambulio hayo yalivuruga mchakato wa upigaji kura kwa saa kadhaa huku wapiga kura wakikimbia ili kuokoa maisha yao.


Eneo hilo la Gwoza, lililopo takriban km103 kusini mwa mji mkuu wa Jimbo la Maiduguri, limekuwa likikumbwa na machafuko ya mara kwa mara ya makundi ya waasi, ambayo huteka watu na kushambulia vikosi vya Serikali vinavyofanya doria uraiani.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad