Staa wa soka wa Argentina na PSG Lionel Messi ametangazwa kuwa Mchezaji bora wa mwaka wa FIFA 2022 huku akiweka rekodi ya kuwa Mchezaji pekee aliyewahi kuingia kwenye kikosi bora cha FIFA cha mwaka mara nyingi zaidi (16) akifuatiwa na Cristiano Ronaldo aliyeingia mara (15).
Tuzo hii ya Messi alikuwa anawania na Wakali wengine kama Karim Benzema wa Real Madrid/ Ufaransa pamoja na Kylian Mbappe wa PSG/Ufaransa.
Tuzo nyingine zilizotolewa leo kwenye usiku wa tuzo za FIFA (FIFA The Best) ni tuzo ya golikipa bora iliyokwenda kwa golikipa wa Argentina na Aston Villa Emi Martinez.
Tuzo ya Kocha bora imeenda kwa Kocha wa Timu ya Taifa ya Argentina Lionel Scaloni, tuzo ya kikosi bora cha mwaka (Courtois, Hakimi, Cancelo, Van Dijk, Modric, De Bruyne, Casemiro, Messi, Benzema, Haaland na Mbappe.